Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa taasisi zilizopewa dhamana ya kusimamia mazao makuu matano ya biashara ambayo ni ya pamba, tumbaku, korosho, chai na kahawa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Amesema mazao hayo ni muhimu sana katika kuwezesha mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano wa kufikia uchumi wa viwanda kwani ndiyo mhimili wa kutoa malighafi za kuendesha viwanda husika na yana mnyororo mpana wa uzalishaji ambao una fursa ya kutoa ajira nyingi.

Waziri Majliwa amesema hayo Septemba 15, 2017 Bungeni mjini Dodoma alipowasilisha hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa Nane wa Bunge. Amesema Serikali imejipanga kuimarisha usimamizi katika uzalishaji na uuzaji wa mazao hayo.

Amesema Serikali itahakikisha kuwa kila taasisi iliyopewa dhamana ya kusimamia mazao hayo, inatekeleza majukumu yake ipasavyo sambamba na kuhakikisha kwamba Watendaji wake wanafanya kazi hiyo kwa uadilifu na ufanisi mkubwa.

“Vilevile, kuwawezesha wakulima kupata mbinu za kisasa za kuyafikia masoko ya uhakika ya mazao yao ili kupata bei nzuri ambayo itawakwamua kiuchumi. Mazao mengine ya kibiashara yatakayotiliwa mkazo ni katani, ufuta, alizeti, mbaazi na ngano.”

Auawa kikatili kisha ubongo wake kuchukuliwa
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 16, 2017