Majeshi yaliyoko ndani ya nchi tano zinazounda Umoja wa Afrika Mashariki yanatarajia kuanza mazoezi maalum kwa ajiri ya kuongeza ujuzi, mbinu na maarifa zaidi katika kupambana na ugaidi, maafa na oparesheni nyingine za ulinzi na usalama.
Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Tawi la Utendaji Kivita na Mafunzo Jeshini, Brigedia Jenerali Alfred Fabian Kapinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku 17 kuanzia Desemba.
Amesema kuwa mafunzo hayo yatafanyikia katika kituo Maalum cha Mafunzo kilichopo, Kunduchi jijini Dar es salaam, ambapo washiriki watakuwa ni Jeshi la Ulinzi Tanzania (JWTZ), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki.
Aidha, zingine ni Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu wa Maafa, Kituo cha Taifa cha Kupambana na Ugaidi, Jeshi la Magereza, Idara ya Uhamiaji na Jeshi la Polisi.