Imeripotiwa kuwa Mwanafunzi aliyepiga picha na kuripoti nyufa kwenye majengo ya mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam amekamatwa na polisi.

Taarifa za kukamatwa kwa mwanafunzi huyo ambaye pia ni kiongozi kwenye serikali ya wanafunzi, Kumbusho Dawson zimethibitishwa na Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi (Daruso), Anastazia Anthony.

“Ni kweli na kwa sasa ndiyo anapelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay. Asubuhi wanahabari walikuwepo hapa na hata watu wa TBA walikuwepo lakini baada ya kuondoka na yeye ndyo akaja kukamatwa,”amesema Anthony

Hata hivyo sababu za kukamatwa kwa mwanafunzi huyo ambaye ni kiongozi chuoni hapo bado hazijafahamika.

 

Video: Mtulia akabidhiwa kadi ya CCM, anena makubwa
Donald Trump ajiondoa mpango wa Umoja wa Mataifa (UN)