Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makasmba amesema kuwa kuna njia mbadala ya kupinga matumizi ya mkaa.
Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa matumizi ya mkaa hayawezi kukomeshwa kwa kupiga virungu watu bali ni kubuni mbinu mbadala ya kuweza kuondoa tatizo hilo.
Amesema kuwa matumizi ya mkaa yamekuwa yakiathiri pakubwa hifadhi za misitu, hivyo jitihada zinahitajika ili kuweza kuokoa hifadhi hizo.
“Asilimia tisini ya miti inakatwa kwasababu ya kutengenezwa mkaa, kwa hiyo ukipunguza matumizi ya mkaa utakuwa umeokoa hifadhi za misitu,”amesema Makamba