Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo kuunda timu ya kufanya ukaguzi wa mali zote za serikali zilizotaifishwa na wajanja ikiwemo maeneo ya wazi, nyumba za umma na kubainisha mikataba yote mibovu inayoinyonya serikali.
 
Ametoa agizo hilo leo wakati wa hafla ya kuwakaribisha wakuu wapya wa wilaya za Kinondoni na Kigamboni, Katibu Tawala Mkoa na kuwaaga wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ambapo amemuagiza katibu tawala kuhakikisha anakamilisha ripoti kabla ya September 03 mwaka huu.
 
Aidha, amewataka watendaji kuhakikisha wanasimamia ipasavyo suala la ukusanyaji wa mapato na kuangalia chanzo kilichopelekea mkoa huo kutofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato pamoja na kufanyia kazi kasoro zilizojitokeza
 
Vile vile Makonda amemtaka katibu tawala kupanga safu mpya ya utendaji kazi ili kuhakikisha wanatatua kero za wananchi ambapo ametaka kuanza na idara ya ardhi, Biashara, Usafi, Mapato na michezo, ambazo bado hazijamridhisha kiutendaji kazi.
 
  • Fahamu sababu 5 za kuchukua likizo kazini
  • Picha: Tayari DC Jokate Mwagelo aapishwa
  • Dondoo 10 za kukuwezesha kuhimili mazingira magumu ya kazi
 
Hata hivyo, amewasihi viongozi walioteuliwa kuchapa kazi ili kuenda sambamba na kasi ya Rais Dkt.John Magufuli aliewaamini na kuwateua

Video: Mkurugenzi wa Twaweza alalama Paspoti yake kushikiliwa na Uhamiaji
Video: Hapi akabidhi Ofisi, atoa neno kwa mrithi wake