Mamlaka ya usimamizi wa hali ya hewa nchini mimetoa angalizo kwa wakazi wa mikoa ya mwambao wa Pwani kuwa mvua kubwa zitaendelea kunyesha hivyo waweze kuchukua tahadhali mapema.

Aidha, Mamlaka hiyo imesema kuwa mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya unguja na Pemba vinatarajiwa kuwa na mvua kubwa inayoambatana na upepo pamoja na mawimbi makubwa.

Taarifa hiyo imesema kuwa hali hiyo inasababishwa na kuimarika kwa ukanda wa mvua nchim na kusababisha kuwepo kwa mgandamizo mkubwa Bahari ya hindi ambayo inasababisha kuwepo kwa mvua kubwa katika ukanda huo.

Hata hivyo, Mamlaka ya hali ya hewa imewataka wakazi wa maeneo husika kuwa na tahadhari pia kuchukua hatua stahiki pindi wanapoona hali isiokuwa ya kawaida.

Magazeti ya Tanzania leo Mei 3, 2017
Video: Wananchi wamtaka JPM kuendelea kutumbua wenye vyeti vya kufoji