Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe hajatangaza kususia chaguzi bali ameona hana uwezo wa kupambana kwa sasa, hivyo ameomba apumzike kwanza ili ajipange upya.
Polepole amesema hayo leo Septemba 21, 2018 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa si mara ya kwanza kwa chama hicho kukimbia chaguzi na wala uamuzi huo haujawarudisha nyuma CCM katika mikakati yao kwani bado kuna vyama vingi zaidi tofauti na Chadema ambavyo vinashiriki chaguzi.
“Huyu Mbowe kutangaza kuwa Chadema imejitoa kwenye Chaguzi zote si mara ya kwanza, kwa hiyo aseme tu kwamba wanaenda kujipanga upya na si kusema kwamba Chadema imejitoa,”amesema Polepole
Septemba 20, 2018 Mbowe wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa chama chake hakitashiriki chaguzi zijazo, akidai kuwa haileti maana yeyote kushiriki chaguzi ambazo haziko huru.
Video: Mbowe afanya maamuzi magumu Chadema