Afisa afya wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa ameagizwa kuhakikisha anakagua usafi wa vyoo na maeneo yanayo zunguka nyumba kwa wilaya nzima ili kujiepusha na ugonjwa wa Kipindupindu katika Wilaya hiyo.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Kamishna Mstaafu Zelote Stephen katika mkutano na wananchi siku ya usafi wa mwisho wa mwezi maarufu kama “Magufuli Day” baada ya Mkuu huyo kukagua nyumba 12, maduka ya wafanyabiashara pamoja na soko katika makao makuu ya wilaya hiyo huku nia ikiwa ni kutaka kujua hali ilivyo wanakojisaidia, wanakohifadhi taka pamoja na hali ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo.

Aidha, aliishauri halmashauri hiyo ya kalambo kuweza kusimamia sharia za usafi zilizopo bila ya huruma ili kuleta mabadiliko na kuitaka halmashauri hiyo kutenga fedha za makusanyo ya ushuru ili kuweza kuboresha hali ya usafi katika mji huo.

“Juzi hapa kulitokea kipindupindu kule Kijiji cha Samazi, hapana hatutaki watu wafe kwa kipindupindu, sasa nimeona choo kinamwaga maji machafu kinyesi kinatoka nje bata wanapokea wanakula, hatupo salama,”

Video: Naibu Waziri wa elimu aagiza walemavu wajengewe vyoo vyao
Magazeti ya Tanzania leo Julai 31, 2017