Mbunge wa Jimbo la Serengeti kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Marwa Ryoba alijikuta katika wakati mgumu mara baada ya wananchi wa jimbo hilo kuanza kumzomea wakati wa ziara ya rais Dkt. John Magufuli mkoani Mara.
Katika ziara hiyo ya rais Dkt. Magufuli mkoani Mara mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chadema, Marwa Ryoba alimtuhumu hadharani mkurugenzi wa wilaya hiyo kwa ubadhirifu wa fedha.
Aidha, mbunge huyo alimtaka rais Dkt. Magufuli kumfukuza kazi mkurugenzi huyo kwa tuhuma za wizi wa mali za umma, huku akijikuta katika wakati mgumu wa kuzomewa na wananchi.
“Mnazomea nini, hata mimi ninaweza kuwa CCM, acheni kunizomea hata mimi ninaweza kuwa ,mwana CCM,”amesema Ryoba
-
LIVE: Rais Magufuli akihutubia wananchi wilayani Serengeti mkoa wa Mara
-
Video: Mimi sikufukuzi mkurugenzi, chapa kazi- Rais Dkt. Magufuli
-
Video: Dkt. Kamani atoa onyo kali kwa viongozi wa vyama vya ushirika