Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Gulamabbas Dewji maarufu kwa jina la Mo Dweji kuendelea kuwekeza nchini na kuitangaza nchi.

Rais Magufuli amesema hayo leo Agosti 1, 2019 jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kusaga nafaka kilichopo chini ya Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL).

Rais Magufuli amemtaka Mo Dewji kutokukubali kurudishwa nyuma na baadhi ya watendaji watakao jaribu kuweka vikwazo kwa wawekezaji.

”Mo Dewji wewe ni bilionea kijana Afrika, chapa kazi, usikubali akukwamishe mtu, uwekezaji huu ni mkubwa sana, kwa hiyo Tanzania iko pamoja na wewe,” amesema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli amewataka watendaji walioko ndani ya serikali kutowavuruga wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiwekeza nchini na kuongeza pato la taifa.

Hata hivyo, Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kumuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa kuwachukulia hatua watendaji wa wizara yake wanao wakwamisha wawekezaji.

Tanzania, Zimbabwe zatiliana saini hati tano za makubaliano ya ushirikiano
Kontena la msaada kutoka China lakutwa likiwa tupu nchini Kenya