Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amebaini madudu katika matumizi ya sh. milioni 393 za ufadhili wa Mfuko wa nchi masikini zaidi duniani (LDCF) chini ya mkataba wa dunia wa mabadiliko ya tabia nchi katika utekelezaji wa mradi wa upandaji na uendelezaji wa mikoko katika delta ya kaskazini ya mto Rufiji.

Katika mradi huo matumizi ya zaidi ya sh. milioni 393  mchanganuo wake hauridhishi huku vikundi vinavyodaiwa kulipwa fedha hizo vikikana kulipwa na kusema hawakuwa na mkataba bali walifanya kazi kama vibarua kwa posho ya sh. 10,000 kila wanapomaliza kazi na hawakuwa na mkataba.

Kutokana na hatua hiyo Mpina amemuagiza Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Makamu wa Rais, Mwatano Maganga kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja anafanya uhakiki wa matumizi ya fedha hizo za mradi na kuelekeza hatua za kuchukua kwakua vielelezo alivyokabidhiwa na Msimamizi wa mradi kutoka Halmashauri ya Rufiji Sabastian Gaganija vina mashaka                                                                                                                                                                                               .

“Naagiza ukaguzi ufanyike, lazima kuna ubadhilifu umefanyika katika utekelezaji wa mradi, baada ya ukaguzi makini, tutajua ukweli na kubaini hatua gani zitachukuliwa.” Amesema Mpina.

Aidha, baada ya zoezi zima la kukagua Delta hiyo yenye kilomota zaidi ya 15 Mpina, amesema amesikitishwa na utekelezaji wa  mradi huo unaotumia  fedha za wafadhili zaidi ya sh.milioni 396 kuwa na madudu na amejionea mwenyewe  kuwa, mradi hauna usimamizi na kusema kuwa,  kuna dalili ya fedha hizo kutumika ndivyo sivyo kwakuwa hata hekta 792 kati ya 1000 zilizodaiwa zimepandwa ni udanganyifu wa wazi.

Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa Rufiji wamesema kuwa  ziara ya Naibu Waziri Mpina, imewasaidia kuweza kutoa changamoto zao katika kukabiliana na uharibifu huo wa Mazingira   na kuiomba Serikali kuongeza usimamizi madhubuti katika mradi huo ili kukabaliana na uharibifu huo wa hifadhi hiyo ya mikoko.

 

 

Idris aweka ‘fumbo’ la alichomfanyia Wema Sepetu alipokuwa Selo polisi
Zinedine Zidane Awapa Somo Real Madrid