Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezitaka halmashauri ambazo shughuli za uvuvi zinafanyika kutenga fedha ili kuweza kupambana na uvuvi haramu.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam mara baada ya kujionea dhana mbalimbali zinazotumiwa na wavuvi haramu, zilizokamatwa na kikosi maalumu cha kupambana na uvuvi haramu.
“Kuanzia sasa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Mkurugenzi anzeni kuwa mnatembea na barua za kufukuza kazi watumishi wanaoshirikiana na wavuvi hawa haramu,”amesema Mpina
Hata hivyo, kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Yohana Budeba ametaja madhara yanayosababishwa na Samaki waliovuliwa kwa kutumia mabomu kuwa ni pamoja na magonjwa ya tumbo na saratani.