Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema amesikizila kero za madereva wa bodaboda wilaya ya Kinondoni jijini humo na kuwaahidi kufikisha jambo hilo kwa rais magufuli, Mrema aliwataka madereva hao kuandika majina ya Polisi na watu wanaojiita polisi jamii wanaochukua rushwa na kuwanyanyasa madereva hao.

Mrema alisema hayo kufuatia malalamiko ya madereva hao wakimueleza kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na watu wanaojiita polisi jamii ambao wamekuwa wakiwakamata bila kufuata utaratibu na wakati mwingine kusababisha ajali. Walisema kuwa watu hao ambao hawana mafunzo ya kipolisi, wakati mwingine huwabambikizia makosa ambayo sio yao bali ni ya abiria.

Jeremy Menez Arejea Ufaransa, AC Milan Wamuachia Kiulaini
Mandanda Amkimbiza Alex McCarthy Selhurst Park