Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kuwa linaendelea na uchunguzi kuhusu watu waliofariki dunia mara baada ya kunywa pombe ambayo inasemekana kuwa ni sumu.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum, Kamanda Lazaro Mambosasa alipokuwa aizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema uchunguzi bado unaendelea hivyo wananchi wajiepushe na unywaji wa pombe haram.
Aidha, amesema kuwa vielelezo vyote vya pombe hiyo wamekabidhi kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili vifanyiwe vipimo kubaini aina ya sumu iliyokuwemo katika kinywaji hicho.
“Inasikitisha kuona biashara hiyo inafanyika wakati tayari ilikuwa imeshapigwa marufuku na eneo hilo tayari liikuwa limebomolewa, nawaasa wananchi wote wanaoishi Kanda Maalum ya Dar es salaam wajiepushe na unywaji pombe haram,”amesema Kamishna Mambosasa.
DC Nzega awashauri wanufaika wa TASAF
-
Video: Familia ya Lissu yamjibu IGP Sirro, Kiama raia wa kigeni
-
Meya wa Jiji la Dar kutegua kitendawili cha mafuriko
Hata hivyo, katika hatua nyingine amesema kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam na hospitali ya Tumbi mkoani Pwani