Jeshi la Polisi Jijini Dar es salaam limekamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali 284, wakiwemo watuhumiwa wa ujambazi sugu, wavuta bangi, wauza gongo na vibaka ambao wamekuwa wakikaba wananchi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Jijini Dar es salaam, Lucas Mkondya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa operesheni hiyo ni endelevu hivyo wahalifu wote waachane na tabia hiyo.

Amesema kuwa wananchi wa Jiji la Dar es salaam wanatakiwa kuondoa hofu kwani jeshi hilo limejipanga vyakutosha kukabiliana na wahalifu huku akiongeza kuwa mtu yeyote atakayejihusisha na uharifu atachukuliwa hatua kali.

“Nawaomba wananchi  watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuweza kutoa taarifa za mahali walipo waharifu tuweze kuwakamata na kuwachukulia hatua stahiki ambapo ni pamoja na kupelekwa mahakamani,”amesema Mkondya.

Hata hivyo, Mkondya amekanusha taarifa ambazo zimezagaa kuwa jeshi hilo lilitumia nguvu kubwa kuwatawanya walemavu waliokuwa wakianda kuelekea katika ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.

Kambi Ya Timu Ya Taifa Ya Ngumi Bado Kizungumkuti
BMT Yabariki Uchaguzi TFF, Latoa Maagizo