Imeelezwa kuwa ukuaji wa uchumi nchini Tanzania unategemea afya bora za wananchi ili kuweza kuongeza ufanisi katika utendaji kazi katika sekta mbalimbali za uzalishaji na ubunifu wa kuijletea maendeleo.

Hayo yamesemwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini William Mkapa wakati wa Sherehe ya kukabidhi nyumba kwaajili ya watumishi wa afya zilizofanyika Chato Mkoani Geita, amesema kuwa amefarijika sana na maendeleo yaliyofikiwa na Wizara ya Afya.

Amesema wananchi hawana budi kila mmoja kujituma na kujikinga na magonjwa mbalimbali pia kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya ili kuweza kuepukana na magonjwa mbalimbali.

“Binafsi nimeridhishwa sana na maendeleo yaliyofikiwa na Wizara ya Afya, tunajua nchi yetu bado ina uhaba wa wataalamu katika sekta ya afya, hivyo mliopo fanyeni kazi kwa weledi kwa kuzingatia haki za binadamu,”amesema Mkapa.

Hata hivyo, Mkapa amezishukuru taasisi zote zinazo shirikiana na Taasisi ya Benjamin William Mkapa kwa kufanya kazi kwa ukaribu zaidi, hali ambayo imesababisha mafanikio makubwa ya ujenzi wa nyumba hizo

Arsene Wenger: Tutasajili Wachezaji Wenye Hadhi Kubwa
Halmashauri zatengewa fedha za dawa kila mwezi