Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amemshukia Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa kutokwenda Nairobi kumjulia hali.

Ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ambapo amesema kuwa mpaka sasa Spika wa bunge hajawahi kwenda kumtembelea.

Amesema kuwa shambulio hilo lilikuwa la kisiasa kutokana na misimamo yake mbalimbali ambayo amekuwa akiisimamia.

“Mimi ni mgonjwa wa Bunge, nikiongozi wa Bunge, ni msemaji wa wizara ya Katiba na Sheria, ni mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, ni mtu mkubwa ndani ya bunge, mpaka leo Spika hajaja kuniona na wala hajatuma mtu yeyote, labda wanasubiri nife ndio waje kwenye mazishi kuniona?,”amesema Lissu

Hata hivyo, Lissu amesema kuwa mpaka sasa bunge halijaonyesha uhusika wake katika matibabu kwakuwa halijatoa hata senti moja kugharamia matibabu ingawa anahaki ya kupata matibabu nje ya nchi.

 

 

 

Mwanajeshi aliyetangaza kumng'oa Mugabe aukwaa uwaziri
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 1, 2017