Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara ameitaka Klabu ya Yanga kutafuta Afisa Habari mwingine atakayeweza kuziba pengo la Jerry Muro.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24Media, ambapo amesema kuwa tangu aondoke Muro klabu hiyo imepoa.

Amesema kuwa vilabu vya Simba na Yanga vinahitaji wasemaji wenye vitu vya ziada ambao wanaweza kuleta hamasa kwa mashabiki.

Aidha, katika hatua nyingine, Manara amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanakerwa na umaarufu wake hivyo hiyo ni sehemu ya kazi yake.

“Unajua kuna kipindi mpaka natamani kuiacha hii kazi ya usemaji, maana kuna watu wanakerwa na umaarufu wangu,sasa mimi umaarufu umenifuata,”amesema Manara

Mnangagwa ajipima ubavu kwa Mugabe, ‘ni mimi au Mugabe’
RC Mghwira alitaka Jeshi la Polisi kujitathmini