Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, mzimbabwe Thabani Kamusoko amezushiwa kifo mara baada ya taarifa kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii.

Taarifa zilisema kuwa Kamusoko amefariki kutokana na ajali iliyohusisha gari aina ya Noah.

Aidha, uongozi wa Yanga kupitia Afisa habari wake, Dismas Ten amekanusha taarifa na kudai kuwa ni za uzushi na tayari wamesharipoti kwenye vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake na kusema kuwa mchezaji wao yuko salama akiwa tayari kwa mechi ya leo dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

“Taarifa hii ni uzushi, mtu huyu amekuwa akifanya hivi mara nyingi kuwazushia watu mbalimbali vifo, alifanya hivyo kwa baadhi ya wachezaji pia kama vile Mrisho Ngasa na Hassan Kessy na vingozi mbalimbali wa Serikali na leo ameandika hivi kwa Kamusoko,”amesema Ten

Hata hivyo, Yanga itakuwa dimbani leo ikimenyana na Gor Mahia ya Kenya, katika mchezo wa wamarejeano kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika utakaopigwa katika dimba la taifa jijini Dar es salaam.

Jokate: Uvumilivu ndio ulionifikisha hapa nilipo
Serikali yakabidhi Pikipiki 21 maafisa elimu Wanging'ombe kurahisisha utekelezaji wa shughuri  za elimu