Hatimaye video ya wimbo wa Joh Makini ‘Don’t Bother’, aliyomshirikisha rapa AKA kutoka Afrika Kusini iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki mzuri  itatambulishwa leo (Novemba 10) katika kituo cha runinga cha MTV.

Video hiyo iliyoongozwa na Justine Campos kwa kiwango cha juu itatambulishwa kama ‘Spanking New’ majira ya saa kumi na mbili za jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Audio ya wimbo huo imetayarishwa na Nahreel ndani ya The Industry.

Kofia Ya 'M4C' Yatajwa Kama Kigezo Cha Kumvua Ubunge Peter Msigwa
Mbweha Wa Jangwani Kuwasili Alkhamis