Watafiti wa sayansi wamebaini kuwa wagonjwa wengi barani Afrika wanapoteza maisha kutokana na kufanyiwa upasuaji, mara mbili zaidi ya takwimu za wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji katika nchi nyingine duniani.

Wanasayansi wao wamesema kuwa vifo hivyo ni matokeo ya usimamizi mbovu wa shughuli za upasuaji na ukosefu wa vifaa vya hospitali na wataalam.

Pia wamegundua kuwa umri wa wagonjwa barani Afrika wanaokufa wakati wakifanyiwa upasuaji ni mdogo zaidi na wanakuwa na afya njema ikilinganishwa na wale ambao hufa wakati wa upasuaji katika mataifa mengine duniani.

Pia, kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyochapishwa katika jarida la kitabibu la Lancet, imeeleza kuwa, idadi ya upasuaji katika nchi za Afrika ni ndogo mara ishirini ikilinganishwa na mahitaji halisi ya upasuaji unaohitajika.


NATESEKA SANA: Mtoto aliyefanyiwa oparesheni 10 tumboni amuomba Rais JPM, Makonda kuokoa maisha yake

Upinzani wampinga Museveni
Mapacha walioungana wafanyiwa uchunguzi zaidi wa kiafya