Wabunge wa upinzani nchini Uganda wamepanga kuwasilisha maombi yao Mahakama ya Katiba kupinga kutumika kwa sheria ambayo inaondoa ukomo wa umri wa kuwania urais.

Sheria hiyo iliyolalamikiwa na wapinzani pamoja na makundi ya kutetea haki za binadamu iliidhinishwa hivi karibuni na Rais Yoweri Museveni.

Kwa sheria hiyo mpya, Rais Museveni aliyechukua madaraka mwaka 1986 ataruhusiwa kuwania  tena katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2021. Mageuzi hayo ya kikatiba yaliondoa kikomo cha umri wa rais.

Wakati huo atakua ametimiza rasmi umri wa miaka 77. Upinzani umekosoa na kupinga mchakato mzima wa ubadilishwaji wa katiba hiyo wakisema mchakato huo ulitawaliwa na hila pamoja na askari waliojihami kuletwa ndani ya bunge kuwadhibiti wabunge waliokuwa wakiupinga mswada huo.

Wabunge hao wamesema wanaendelea kujipanga ili kufikisha hoja zao katika Mahakama ya Katiba. Hata hivyo, hawakutaja ni lini watafikisha hoja hiyo mbali ya kusisitiza kuwa itafikishwa wakati muafaka.

Mashinji ataja sababu za viongozi kuhama Chadema
Vifo vingi hutokea wakati wa upasuaji Afrika