Taarifa kutoka Wizard ya Afya nchini Uzbekistan, imesema takriban watoto 18 wamefariki dunia baada ya kudaiwa kunywa dawa ya maji iliyotengenezwa na mzalishaji wa dawa kutoka India, Marion Biotech.
Taarifa hiyo, imeeleza kuwa watoto 18 kati ya 21 waliotumia syrup ya Doc-1 Max wakiwa na ugonjwa wa kupumua kwa papo hapo walikufa baada ya kuinywa, huku Wizara ikisema sawa hiyo ni dutu na yenye sumu.
Imesema, Dawa hiyo iliingizwa nchini Uzbekistan na Quramax Medical na ilitolewa kwa watoto nyumbani bila agizo la daktari, wazazi, ushauri wa wafamasia, na kipimo kilichozidi kiwango cha kawaida cha watoto.
Hata hivyo, Marion Biotech, Quramax Medical na Wizara ya Afya ya India bado hazijatoa tamko juu ya tuhuma hiyo ingawa chanzo kimoja cha Habari toka Serikali ya India kilisema Wizara ya Afya inachunguza suala hilo.