Baadhi ya Viongozi waliokuwa wakimuunga mkono Raila Odinga, katika kinyang’anyiro cha ugombea Urais nchini Kenya wameanza kukubali kushindwa kutokana na kasi ya utoaji wa matokeo inayoendelea kuonesha William Ruto anaongoza.
Viongozi hao, ambao pia ni wandani wa karibu wa rais Uhuru Kenyatta akiwemo Amos Kimunya na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama cha Jubilee, Kanini Kega waliamua kuunga mkono juhudi za Odinga wakiamini uwepo wa uwezekano wa kupoteza viti vyao kutokana na wasifu wa chama cha UDA eneo la Mlima Kenya.
Wengione ambao waliamua kuunga juhudi ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee, Jeremia Kioni ambaye anakuwa ni miongoni mwa Viongozi waliokubali kushindwa baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Chama cha UDA kinachoongozwa na William Ruto kiliamua kuwafukuza Viongozi wote wa eneo hilo waliokuwa wakimuunga mkono Raila Odinga, ambaye ni mgombea wa Muungano wa Azimio kitu ambacho hawakukubaliana nacho.
Kwa upande wa Chama cha Jubilee cha Uhuru Kenyatta, chenyewe kilikuwa na wagombea wengi waliowania na wengine kutetea viti vyao katika eneo la Mlima Kenya, na sasa wanasema wapinzani wao tayari wamechukua uongozi wa maeneo mengi kutokana na zoezi la hesabu za kura linaloendelea.