Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amewataka Vijana nchini kuacha tabia ya kuuza viungo vyao vya mwili hususani figo, ili kuepukana na madhara ya kiafya.

Dkt. Mpango ametoa wito huo akiwa katika ziara mkoani Ruvuma, mara baada ya kuzindua jengo la kutolea huduma ya usafishaji figo lililopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Joseph, Peramiho.

Aidha, ameongeza kuwa utoaji wa figo unaweza kuhatarisha maisha eandapo figo moja iliyobaki ikishindwa kufanya kazi kwa ufanisi na kuwataka watanzania kuwa na utaratibu wa kupima afya ili kuepukana na hatari za maradhi mbalimbali na kufikia hatua mbaya zaidi..

Hata hivyo, Makamu wa Rais pia ameshauri kuachana na ulaji usiofaa, unywaji wa pombe kupitiliza pamoja na kuhimiza kufanya mazoezi kuepukana na hali hiyo.

Amani, mshikamano ni nguzo ustawi wa Taifa - Majaliwa
Mvutano waibuka zuio Wanawake kusafiri bila Mwanaume