Tasisi isiyo ya kiserikali Babawatoto Organazation imeungana na mataifa mbalimbali kuadhimisha siku ya vijana dunia lengo ikiwa ni kupaza sauti kwa niaba ya vijana hasa katika maendeleo ya vijana na haki zao kidunia na kitaifa pia kauli mbiu ikiwa ni Ushirikishwaji wa Vijana Utekelezwe Kidunia.
Akizungumza na waandishi wa habari katikia maadhisho mkurugenzi wa Taasisi ya Babawatoto Alfayo Wangwe amesema kupitia sera ya vijana ya mwaka 2007 kila kijana anaitajika kufikiwa na maendeleo na kuwezeshwa kutimiza ndoto zao.
Amesema kama Taasisi hiyo inafanya kazi kwa kuzingatia makundi yote ikiwemo kundi la vijana wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapa huduma mbalimbali za kijamii na kutimiza ndoto zao kwa kuwapa mafunzo ya fani mbalimbali na kupewa vitendea kazi, kuondokana na maisha ya mtaani.
Kwa upande wake afisa vijana Manispaa ya Ilala Sapiencia Masaga amewaasa vijana kuvaa jukumu la kuwajibika kama kijana hasa katika kushiriki mikutano mbalimbali ya serikali ili kuwa na nafasi ya kushilikishwa kama kauli mbiu inavyosema “Ushirikishwaji wa Vijana Utekelezwe Kidunia”.
Aidha vijana wa Babawatoto Organazation waliadhimisha siku ya vijana kwa kufanya mjadala ni jinsi gani kijana anaweza kushirikishwa kwenye uongozi na pia walipata semina kuhusu haki ya kijana katika kushilikishwa kwenye nyanja mbalimbali.