Tetemeko la Ardhi lenye nguvu ya 5.9 limetikisa katika baadhi ya maeneo ya jiji la la Dar es Salaam leo, Agosti 12, 2020.

Akitoa ufafanuzi kuhusu tetemeko hilo, Mkuu wa Idara ya Jiolojia wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Elisante Mshiu, amesema kuwa tetemeko hilo lina ukubwa sawa na tetemeko lililoukumba mkoa wa Kagera Septemba 10, 2016.

“Kwa hakika hilo ni tetemeko la ardhi, na kwa mujibu wa vipimo vyake inaonesha lina nguvu ya 5.9. Hii ni tetemeko ‘almost’ sawa na lile lililotokea Kagera,” Dkt. Mshiu ameiamba Azam TV.

Imeelezwa kuwa tetemeko hilo limetokea takribani kilometa 82 kusini mashariki mwa mwambao wa Dar es Salaam.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeeleza kuwa tetemeko hilo halikutarajiwa, lakini itatoa taarifa kamili mapema kesho.

Mwaka 2016, tetemeko lenye nguvu ya 5.9 kwenye skeli ya MMS lililotokea takribani Kilometa 40 chini ya uso wa ardhi. Tetemeko hilo lilianzia katika Kata ya Nsunga, karibu na mpaka wa Tanzania na Uganda.

Endelea kuwa karibu na Dar24 Media, tutakujuza kwa undani tukikuunganisha na TMA na vyanzo vingine.

DC atoa neno kuhusu Uchaguzi Mkuu

TAMWA: wasisitiza uchaguzi huru na haki

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 13, 2020
TAMWA: wasisitiza uchaguzi huru na haki