Scolastica Msewa – Kibaha.

Makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango amewataka Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa nchini kushughulikia kwa kutatua kero za malalamiko ya Wananchi kwa wakati badala ya kuacha hadi wakaanza kupaza sauti wenyewe wakitafuta utatuzi wa kero zao ngazi taifa.

Dkt. Mpango ameyasema hayo mjini Kibaha, wakati akifungua Mafunzo ya wiki moja ya uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu tawala wa Mikoa Tanzania bara yaliyofadhiliwa na Bank ya NMB kwa agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuboresha, kuongeza stadi kazi na ujuzi wa utendaji kazi katika kumsaidia Rais kuhudumia Wananchi.

Amesema “kumekuwa na kuchelewa kwa utatuzi wa migogolo wa Wananchi ambako hupelekea Wananchi kupaza sauti zao wao wenyewe kwa kupeleka malalamiko ya ngazi za juu wenyewena hupelekea wao wenyewe kutafuta utatuzi wa kero zao ngazi za juu.”

Aidha, Dkt. Mpango amesema ni muhimu Viongozi hao kufahamu utendaji wa serikali za mitaa na serikali kuu jinsi inavyohudumia Wananchi pasipo muingiliano wala migogolo aliitaja baadhi ya mifano ya upungufu wa kiutendaji kuwa ni pamoja na kuwepo kwa kutokuzingatia mipaka ya kiutendaji katika ya Wakuu wa mikoa na Makatibu tawala wao ambayo ni kinyume cha taratibu, sheria na kanuni zilizopo.

Awali akimkaribisha Makamu wa Rais huyo Waziri wa Ofisi ya nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki alisema Mafunzo hayo ya wiki moja Wakuu hao wa mikoa na Makatibu tawala wa mikoa watafundishwa masomo 20 na wawezeshaji wabobezi waliowahi kufanya kazi serikalini kwa muda mrefu.

Alisema tayari mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Makatibu tarafa yanaendelea ambapo wanafundishwa kwa awamu kwa kugawanyishwa kwenye Kanda za mikoa nchini Hadi watakapo kamilika wote nchi nzima huku Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais menrjimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete amesema mafunzo hayo yatasaidia kuboresha wa Umma na Utawala Bora katika mikoa nchini.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 23, 2023
Rais Samia aridhia ufufuaji kituo mafunzo ya Kilimo