Nyota wa Klabu ya Villarreal Alex Baena amemfungulia mashtaka kiungo wa Real Madrid, Federico Valverde kufuatia kumpiga ngumi usoni katika eneo la maegesho ya magari baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania uliozikutanisha timu hizo mwishoni mwa juma lililopita.

Hata hivyo, Valverde ataepuka adhabu kutoka mamlaka za soka nchini Hispania ikiwemo kufungiwa michezo 12 ya Ligi ‘La Liga’ kwa sababu Villarreal imeamua kutoripoti tukio hilo kwenye Shirikisho la Soka la nchi hiyo, vile vile ripoti ya mwamuzi haikujumuisha tukio hilo.

Lakini Villarreal imethibitisha katika taarifa yake iliyotolea juzi Jumapili (April 09) kwamba polisi watahusishwa na kufanyia uchunguzi tukio hilo lilitokea baada ya mchezo ambao Real Madrid ilipokea kichapo cha mabao 3-2.

Valverde alichukizwa kufuatia kauli iliyodaiwa kutolewa na mchezaji huyo wenye umri wa miaka 21, kuhusu familia yake mapema mwaka huu, hata hivyo mchezaji huyo alikanusha kutoa kauli hiyo.

Taarifa za uhakika zinadai Baena alimwambia Valverde atokwe machozi kwa sababu mpenzi wake hatajifungua mtoto kutokana na mimba kuharibika.

Kauli hiyo anaiwa kuisema baada ya mchezo uliopita wa Kombe la Mfalme ‘Copa del Rey’ uliozikutanisha timu hizo mwezi uliopita.

Marcus Rashford hali tete Man Utd
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo April 11, 2023