Licha ya Serikali kushusha viwango vya bei za nyumba za Magomeni Kota, Kaya 644 zimeendelea kususia bei hiyo zikidai kuwa ni kubwa na haziendani na hali halisi ya kipato chao huku wakiiomba Serikali huku Mwenyekiti wa Wakazi hao, George Abel akisema hawatoanza kuzilipia nyumba hizo.
Abel amesema, bei ya awali iliyopendekezwa na Serikali ilikuwa ni Shilingi 12 milioni hadi Shilingi 17 milioni, lakini wanashangaa wahusika kuongeza kiwango tofauti na mapendekezo ya awali.
Februari 2023 Mtendaji Mkuu wa TBA, Daudi Kandoro alisema nyumba hizo zilikuwa zikiuzwa Shilingi 74 milioni kwa chumba na sebule na Shilingi 86 milioni kwa vyumba viwili na sebule, lakini kwa kuzingatia vipato vya kaya hizo, walipunguza hadi Shilingi 48 milioni na Shilingi 56 milioni.
Nyumba hizo zilivunjwa mwaka 2009 na Wananchi hao waliahidiwa kukaa bure kwa miaka mitano na baadaye kuzinunua kwa bei nafuu.