Kufuatia Serikali ya Myanmar kuvipiga marufuku vyama 40 halali vya kisiasa kabla ya uchaguzi wake uliokataliwa, Kampeni ya Burma UK (BCUK), imetaka vikwazo dhidi ya Myanmar vitekelezwe ipasavyo na kwa haraka.

Hatua hiyo inafuatia hatua iliyochukuliwa Machi 28, 2023, jeshi la Myanmar lilitangaza kuwa limepiga marufuku vyama 40 vya kisiasa, ikiwa ni pamoja na cha National League for Democracy (NLD), ambacho kimekuwa kikishinda kila uchaguzi wa nchi hiyo.

Vikosi vya usalama Nchini Mynamar vikiwa katika doria. Picha ya Anadolu Agency.

Aidha, marufuku hiyo inafuatia jeshi kutaka vyama vya siasa visajili upya, au kujiandikisha kwa mara ya kwanza, na Tume ya Uchaguzi ya Muungano iliyoteuliwa na jeshi, jambo ambalo vyama hivyo vilikataa kufanya kwa vile jeshi halina uhalali wala nguvu za kisheria za kuweka kanuni za uchaguzi.

Wanajeshi wa Burma wamekuwa wakiwakamata, kuwaua, kuwafunga jela na kuwatesa wanachama wa NLD, na kufunga ofisi zao, lakini hawajafikia hatua ya kuweka marufuku huku wakikabiliwa na upinzani mkali baada ya jaribio lao la mapinduzi kuanza miaka miwili iliyopita.

Basi la chuo cha Pwani lapata ajali, 18 wafariki
Uganda kupeleka Wanajeshi wake kuilinda Moscow