Watu 14 wakiwemo wanafunzi, wamefariki dunia baada ya Basi la chuo kikuu cha Pwani kuligonga gari la abiria aina ya matatu nchini Kenya, ajali inayotokea wakati mamlaka ikiendesha kampeni ya usalama barabarani ya kuwataka madereva kuchukua tahadhari, hasa katika msimu wa mvua unaoendelea.

Mkuu wa Polisi wa Bonde la Ufa, Tom Odera ajali hiyo imetokea Machi 30, 2023 magharibi mwa mji mkuu wa Nairobi, ambapo watu 12 walifariki papo hapo, na wengine wawili walifariki wakiwa njiani wakati wakipelekwa Hospitalini.

Amesema, basi hilo lililokuwa likielekea Nakuru kutokea jijini Nairobi, lilikuwa limebeba watu 30 na ameongeza kuwa huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka na kwamba lilipata ajali baada ya dereva kupoteza mwelekeo, kuligonga gari lililokuwa likija mbele na kubingiria kwenye mtaro.

Ajali za barabarani katika barabara za Kenya zimekuwa ni kawaida, ambapo wiki iliyopita, Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama ilisema watu 974 walikufa katika ajali za barabarani kote nchini tangu mwezi Januari.

Wizara yataka kasi utoaji chanjo watoto chini ya miaka mitano
Serikali yafuta vyama 40 vya siasa, wapinzani wataka vikwazo