Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amewasili nchini na kupokelewa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt Phillip Mpango ambapo anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili.

Ziara hiyo, inatokana na mwaliko wa Rais wa  Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Kamala walipokutana Jijini Washington mwaka 2022 wakati wa ziara yake ya kikazi nchini Marekani, ambayo pia ilihusisha uzinduzi wa Filamu ya ‘The Royal Tour’.

Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris akisalimiana na Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango mara baada ya kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Ziara yake Barani Afrika, ilianzia nchini Ghana kabla ya kuwasili nchini na kutoka hapa anatarajia kwenda nchini Zambia, ambapo atazungumzia maendeleo ya kiuchumi, mabadiliko ya tabia nchi na usalama wa chakula.

Hata hivyo, kuwasili kwa Kamala nchini ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Rais wa Marekani, Joe Biden Desemba 2022 wakati wa mkutano kati ya Marekani na Viongozi wa nchi za Bara la Afrika.

Mradi ufugaji Nyuki kuvinufaisha Vijiji Kigoma
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 30, 2023