Viwanja vya ndege 208 hapa nchini vimefungiwa na mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania (TCAA), baada ya kushindwa kufuata kanuni za usafiri wa anga.

Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo (TCAA), Hamza Johari ametangaza kuvifungia viwanja hivyo vidogo baada ya kubainika kushindwa kufuata kanuni za usafiri wa Anga.

Kanuni hizo zinakataza uendeshaji wa viwanja vya ndege bila kupata usajili au leseni inayotolewa na TCAA na ni kosa ambalo huadhibiwa kisheria ambapo viwanja hivyo vimeondolewa katika rejista ya viwanja vya ndege na havitaruhusiwa kutumika bila idhini ya TCAA.

Aidha Johari amesema mnamo mwezi Mei 6 mwaka huu TCAA ilitoa muda hadi desemba 2019 kwa wamiliki au waendeshaji wote wa viwanja vidogovidogo vya ndege kutimiza matakwa ya kanuni na kusajili au kupata leseni.

 

Hukumu yatolewa mauaji ya khashoggi , Majina ya wauaji yafichwa
Serikali yakemea uharibifu wa miundombinu kufanikisha biashara ya chuma chakavu