Wimbi la kuhama vyama kwa wanasiasa mbalimbali nchini limezidi kuwachanganya wananchi kiasi cha kushindwa kutambua Chama kipi kinafaa au kiongozi gani mwenye msimamo kisiasa.
Hayo yamebainishwa na wananchi mbalimbali, ambapo wamesema kuwa wimbi la kuhama hama vyama linazidi kuwavuruga na kuwafanya washindwe kuelewa kiongozi yupi yuko sahihi.
Aidha, wamesema kuwa siasa za sasa zimetawaliwa na mihemuko ambayo inapelekea mtu kuchukua maamuzi bila kuwafikiria wapiga kura wake waliomchagua.
“Sihitaji kushabikia mtu kwasasa, maana unashabikia mtu na chama fulani ghafla siku mbili unamuona kaondoka kaenda chama kingine, na wewe unahama, ukifika huko baada ya muda naye anahama sasa unashindwa kufahamu ufanye nini, kwakweli CUF, CCM na CHADEMA wanatuchanganya sana kwasasa,”amesema Aisha
Hata hivyo, siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi kubwa la wanasiasa kuhama vyama vyao, hivyo kuwaweka katika hali ya sintofahamu wafuasi wao.