Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amempa wosia Mwenyekiti mpya wa  (UVCCM), Kheri James kuwa amepata nafasi hiyo hivyo aitumie vizuri kuhakikisha UVCCM wanakuwa waasi wa udhalimu wa serikali na viongozi mbalimbali.

Amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo ameandika kuwa wao walijaribu kufanya hivyo lakini walishindwa lakini anaamini kutokana na uwezo wa Mwenyekiti huyo wa UVCCM anaweza kutimiza hilo.

“Sisi kaka zako tulishindwa ndani ya mioyo yetu tunajua tulishindwa kufanya vizuri bali tutakupa ushirikiano kwenye kutimiza wajibu Wako,”amesema Bashe

Hata hivyo, Mbali na hilo Bashe amemsisitiza Mwenyekiti mpya wa UVCCM kuwa imani aliyopewa na vijana ahakikishe anaitumia vizuri na asimuangushe Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye aliwataka vijana kufanya mabadiliko ya viongozi ambao wataleta mabadiliko ndani ya chama na Umoja huo wa vijana.

 

Lissu: Nitadai haki mpaka mwisho wa maisha yangu
Serikali yatangaza mnada wa madini ya Tanzanite