Wafuasi wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance, wameandamana kupinga kukatika kwa umeme kunakoendelea nchini Afrika Kusini, wakisema hali inazorotesha uchumi wa nchi na maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Kukatika kwa umeme nchini humo, kunatokana na tatizo la nishati kwa zaidi ya muongo mmoja, na sasa limeongekeza zaidi hasa kwa mwaka huu wa 2023, ambapo ratiba ya umeme hukosekana kwa kila siku na wakati mwingine kwa muda wa saa kumi.
Shirika la umeme la Serikali, ESKOM linatajwa kuwa na madeni huku likikabiliwa uchakavu wa mitambo ya makaa ya mawe inayokaribia kuharibika.
Hata hivyo, inaarifiwa kuwa suala la rushwa na hujuma pia limelidhoofisha shirika hilo kwa kiasi kikubwa na Mkurugenzi Mtendaji, Andre de Ruyter anatazamiwa kuacha kazi mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu (2023).