Uanzishwaji wa mkakati wa Polisi kata, ulikiwa na dhamira ya kushirikiana na watendaji wa kata kutafuta taarifa za uhalifu na kuzifanyia kazi katika maeneo yao, ikiwa ni Pamoja na kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kijnsia.

Hayo yamesemwa hii leo Januari 26, 2023 na Kamishina wa Polisi Kamisheni ya Polisi jamii, Faustine Shilogile wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kilimanjaro, wakaguzi kata na watendaji wa kata.

Amesema, Jeshi hilo lilihakikisha kuwa Tanzania bara na visiwani kunakuwa na askari kata ambaye atashirikiana na watendaji wa kata kuhakisha jamii ya eneo husika inaishi kwa amani na utulivu, kwa kutafuta taarifa za uhalifu na wahalifu katika kata husika.

Shilogile ameongeza kuwa, Polisi pia imeweka utaratibu huo ikiwa ni sehemu ya kuweka ukaribu wa askari wa Jeshi hilo na wananchi ikiwa ni mpango wa kutatua na kushiriki katika mswala ya kijamii.

Wataalam mipango miji waonywa utwaaji ardhi bila kushirikisha Wananchi
Waandamana kupinga kukatika kwa umeme