Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete amewataka Wataalam wa Mipango miji kutambua kuwa zoezi la utwaaji Ardhi ni la ushirikishwaji tofauti na baadhi ya wataalam wanavyofanya bila kushirikisha Wananchi.

Kikwete, ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya usajili wa wataalam wa Mipango miji na kuwaonya wataalam hao, kukiuka taratibu za kitaaluma hali inayopekea wanasiasa kungilia kati kutoa maamuzi yanayoweza kuchochea migogoro.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Manajimenti ya Wizara mara baada ya kuzindua bodi hiyo leo Jijini Dodoma.

Amesema, vitendo hivyo havikubaliki na kuitaka bodi ya wataalam wa mipango miji kutoa elimu kwa wataalam hao, kuacha tabia hiyo inayochangia kuleta migogoro kwa wananchi hasa katika maeneo ya miji, ambapo miradi ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi imekuwa ikiendelea.

Aidha, Ridhiwani pia ameonya tabia ya kutosimamia mipango miji waliyoiweka inasababisha miji kuvurugwa kwani kwasasa kila mahali kuna ujenzi wa vyumba vya maduka au vituo vya mafuta na baa katika makazi ya watu.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 27, 2023
Watendaji Kata waaswa kuwatumia Polisi kukabili uhalifu