Polisi mkoani Kilimanjaro, inamshikilia mtu mmoja, Shukuru Nguma ambaye ni mkazi wa kijiji cha Komela kilichopo Wilayani Moshi, kwa tuhuma za uwalawiti kwa nyakati tofauti wanafunzi 18 wa shule tofauti za msingi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema taratibu za uchunguzi juu ya tuki hilo zinaendelea na kwamba mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani na kwamba Shukuru anashikiliwa katika kituo cha Polisi Himo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Abbas Kayanda akizungumzia tukio hilo amesema Shukuru alikamatwa Januari 21, 2023 baada ya kuzagaa kwa taarifa na ndipo timu ya uchunguzi ilitumwa kijijini hapo kujiridhisha ukweli wa tuhuma hizo.

“Tumefuatilia tumebaini ni kweli hii ni baada ya kutuma timu yetu kuchunguza na Serikali tayari imeshachukua hatua ikiwemo kumkamata tumeshakamilisha taratibu zote ili tumfikishe mahakamani,” alisema Maigwa.

Waandamana kupinga kukatika kwa umeme
Wafugaji 27 wafariki kwa kulipukiwa na bomu machungani