Waasi wa M23 waliopo mashariki mwa DRC, wanawashikilia mateka raia wanaoshukiwa kushirikiana na wanamgambo adui, huku mapigano yakizuka licha ya juhudi za amani za hivi karibuni, vyanzo vya ndani vimeiambia AFP Jumatatu.

Kundi hilo, liliteka maeneo kadhaa kutoka kwa jeshi la serikali na washirika wake wanamgambo katika jimbo la Kivu Kaskazini katika miezi ya hivi karibuni na lilisonga mbele kuelekea mji wa Goma.

Hata hivyo, lilikabidhi mji wa kimkakati wa Kibumba kwa kikosi cha Afrika Mashariki wiki iliyopita baada ya shinikizo kubwa la kimataifa kulitaka kusitisha mapigano, likisema hatua hiyo ilikuwa “ni ishara ya nia njema kwa ajili ya amani.”

Kikosi cha Waasi wa M23 katika harakati za mapambano. Picha ya Alliance.

Jeshi la Congo lilipuuza kuondoka huko na kusema ni “ulaghai” unaolenga kuimarisha ngome za kundi hilo kwingineko na vyanzo vya usalama vimeiambia AFP kwamba mapigano yalizuka tena Jumapili huko Kivu Kaskazini.

Mwakilishi wa mashirika ya kiraia katika eneo hilo, Cyprien Ngoragore amesema awali Waasi hao waliwakamata karibu watu 50 wanaotuhumiwa kushirikiana na makundi mawili ya wanamgambo wapinzani wa M23 ndani na karibu na eneo la Tongo.

Wajadili marufuku ya wanawake kufanya kazi taasisi binafsi.
Idadi waliokufa na theluji yafikia watu 50