Wakazi wa jimbo la Sudan Kusini la Kordofan wanaripoti kukusanyika kwa kundi kubwa la waasi hapo jana Alhamisi na hivyo kuzusha wasi wasi kwamba mapigano yanayoendelea nchini humo yanaweza kuenea hadi upande wa kusini mwa nchi.
Waasi hao ni wa kundi la SPLM –N linaloongozwa na Abdelazizi al-Hilu na wanakadiriwa kufika maelfu ya wapiganaji wenye silaha nzito nzito na bado haijafahamika ni upande gani wataungana nao katika mapigano yanayoendelea.
Wakazi hao wanasema Wapiganaji wa SPLM-N wamekusanyika katika kambi za kijeshi karibu na Kadugli, mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kusini , na kusababisha jeshi la taifa kuimarisha vita vyake na kudai kuwa wapiganaji wa RSF wamefunga barabara ya kaskazini na kuzuia usafiri wa bidhaa.
Aidha, wamesema kwa akili ya kawaida ukusanyikaji huo unaashiria wapiganaji hao wanajiandaa kuongeza nguvu upande wowote watakaoungana na na hivyo kuzusha hofu ya kusambaa kwa mapigano nchi nzima ya Sudan.