Wabunge nchini Uganda wamejiongezea mishahara kwa asilimia 39, asilimia 15 wameongezewa wafanyakazi wote wanaosiadia kuendesha shughuli za bunge, kwa madai ya kuendana na ongezeko la gharama za maisha.
Benki ya Uganda mwezi uliopita ilitangaza mtikisiko wa uchumi nchini humo ambao umepelekea ongezeko la bei kwa bidhaa muhimu kama vyakula na nishati kwa asilimia 3.
Mbunge Peter Ogwang, amesema jana usiku kuwa mshahara wao wa awali ulikuwa hautoshelezi kwa mahitaji ya kawaida ya wabunge.
Wabunge hao pia wamejiongezea pesa ya usafili wa ndani na ule wa nje ya nchi, na bado wanaomba serikali iwaongezee Shs 20.4b kwaajili ya kamati za pembeni na safari zake.
Licha ya kuwa Rais Museveni aliwapa onyo wabunge wapya 2016 walipokuwa ikulu juu ya kugombania safari na kuzunguka duniani kama baadhi ya wavumbuzi wa karne ya 15 kutoka italia, ila wawekeze muda wao kutumikia wannchi wa Uganda bado safari wameendela kuzipa kipao mbele.
Aidha msemaji wa wizara ya fedha nchini Uganda Jim Mugunga, jana jioni amesema hawakuwa na taarifa yoyote juu ya ongezeko la mishahara ya wabunge na wafanyakazi wa bunge.
-
Rais wa Ufaransa ajibu maandamano ya vizibao vya njano
-
Rais Putin kuwakutanisha Kim Jong Un na Rais Trump kuhusu Nyuklia
-
Viongozi wakuu wa Baraza la Mpito la Kijeshi wajiuzulu Sudan