Taasisi zinazohusika na uwekezaji zimetakiwa kutoa kipaumbele zaidi kwa
fursa za Bunifu za wabunifu ambazo ziko tayari sokoni ili kuwavutia
wengi zaidi kuibua na kutangaza kazi zao za kibunifu kwa manufaa ya
nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye mashindano ya kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu Jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa Sayansi na Teknolojia, Dokta Amos Nungu amesema kuwa katika utekelezaji mashindano hayo yanaangalia mambo matatu ambayo ni
kuibua wabunifu,kuwatambua na kuwezesha wabunifu ikiwemo kuwaendeleza kupitia kazi zao.
Aidha, Nungu ameongeza kuwa ni kwa miaka miwili mfululizo COSTECH imekuwa ikiweka mazingira wezeshi kwa wabunifu kuhakikisha bunifu za wabunifu zinaibuliwa na kuboreshwa zaidi ili ziweze kutambulika Kitaifa na Kimataifa.
Amesema wabunifu wanatakiwa kupewa mbinu mbalimbali ambazo zitawawezesha kuingia sokoni.