Wafuasi wa Muhubiri Ezekiel Odero wa kanisa la New life International Mavueni kaunti ya Kilifi, wameamua kufanya ibada nje ya Mahakama ya Shanzu kaunti ya Mombasa wakidai wanamuombea Kiongozi wao.

Kwa mujibu wa baadhi ya wafuasi hao, wamesema wamechukua hatua ikiwa ni sehemu ya harakati za kumuombea Mhubiri huyo ambaye amekamatwa kwa tuhuma ambazo wanasema ni za kusingiziwa.

Waumini hao wakiwa nje ya Mahakama kushiriki ibada.

Mchungaji huyo, (Ezekiel Odero), alikamatwa na Polisi akituhumiwa kwa mauaji ya watu 98 ambao ni waumini wa Kanisa la Good News International Ministry la Mchungaji Paul Mackenzie na kufikishwa Mahakamani hapo.

Odero amekuwa kizuizini kwa zaidi ya wiki moja sasa na leo Mei 2, 2023 kesi hiyo ilitarajia kutajwa tena akihusishwa pia na vifo vingine vilivyotokea katika Kanisa lake baada ya kushawishi waumini wake kutorosha ndugu zao wagonjwa waliokuwa Hospitali na kuwapeleka kwake ili awaombee.

John Bocco: Kilichobaki ni halali yetu
Rais Samia amerejesha matumaini ya Watanzania - NGOs