Mji wa kusini-mashariki wa Tunisia wa Zarzis, umekumbwa na taharuki baada ya maduka na ofisi za serikali na vituo vya afya kufungwa, kutokana na Waandamanaji kutaka msako upya wa kuwatafuta jamaa waliotoweka, huku wakiimba nyimbo za kutaka ukweli, na maelfu wakiingia mitaani kuweka shinikizo kwa mamlaka lililomfanya Rais kumtaka Waziri wake wa Sheria afungue uchunguzi.

Mmoja wa wandamanaji, Ezzedine Msalem mesema, “Serikali lazima ifichue ukweli kuhusu uhalifu ambao ulifanywa dhidi ya wakazi wa Zarzis kwa maziko ya miili iliyopatikana baharini inayoaminika kuwa abiria kutoka kwenye mashua katika makaburi ya wahamiaji wa kigeni bila kuwatambua hapo awali, wala kufanya uchambuzi wowote wa DNA.”

Wiki nne zilizopita, Watunisia 18 walipanda boti kuelekea Italia, kabla ya kuzama na watu wanne, wanaoshukiwa kupotea ambao ni Watunisia, walizikwa katika makaburi ya karibu ya wahamiaji wa kigeni bila juhudi za kuwatambua na sasa miili hiyo imetolewa kwa ajili ya kutambuliwa, huku miili mingine miwili inayoaminika kuwa ya Watunisia ikipatikana.

Moja ya vyama vikubwa nchini humo, ambalo ni shirikisho la vyama vya wafanyakazi UGTT, lilionyesha kuunga mkono mgomo huo na kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu juhudi za uokoaji na jinsi miili hiyo ilivyozikwa huku Umoja wa Haki za Kibinadamu wa Tunisia ukisema mamlaka hazijatoa rasilimali zinazohitajika katika shughuli za utafutaji na uokoaji kwa wakati unaofaa.

Wizara ya ulinzi nchini Tunisia, imesema mwishoni mwa juma iliwakamata karibu wahamiaji 200 waliokuwa wakijaribu kufika Ulaya na kulingana na takwimu rasmi zaidi ya wahamiaji 22,500 wamezuiliwa tangu kuanza kwa mwaka huu, ambapo nusu ya hao ni kutoka Afrika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Makahaba waitaka Mahakama itende haki mauaji ya wenzao sita
Hakuna wa kunipiga marufuku: Mtoto wa rais ajibu