Serikali nchini, imesema mafunzo ya kuwajengea uwezo kiutendaji Viongozi katika Utumishi wa Umma na sekta binafsi yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi yamelenga kuunga mkono jitihada za Serikali za kuimarisha Utawala Bora nchini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi ameyasema hayo hayo jijini Dar es Salaam, katika Kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, wakati akizindua awamu ya tatu ya Programu ya mafunzo kwa Viongozi.

Amesema, program zote za mafunzo zinazotolewa kwa viongozi kupitia Taasisi ya UONGOZI zimelenga kuimarisha uwezo na kuwaongezea ufanisi kiutendaji kwenye maeneo yao ya kazi na kwamba zinalenga kuimarisha uwezo wa kufanya maamuzi ya kimkakati, kuongoza rasilimaliwatu na kujenga sifa binafsi za kiongozi.

Aidha, Ndejembi ameongeza kuwa, mafunzo hayo ni muhimu katika kuimarisha utawala bora utakaokuwa ni chachu ya kuleta maendeleo endelevu nchini na kuwataka washiriki kuyazingatia kikamilifu ili kupata elimu na ujuzi utakaowaongezea ufanisi kiutendaji na kuleta mabadiliko chanya katika maeneo yao ya kazi.

Kwa upande wake, mshiriki wa mafunzo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Afya Plus, Dkt. Pastory Sekule amesema baada ya kuhitimu anatarajia kupata uzoefu utakaomuwezesha kusimamia rasilimali, pamoja na mabadiliko kwa kuwaongoza watumishi alionao eneo lake la kazi.

Jumla ya washiriki 68, kutoka katika taasisi za umma na sekta binafsi wanashiriki mafunzo hayo ya awamu ya tatu ya Program ya Mafunzo kwa Viongozi yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi kwa ushirikiana wa Serikali ya Finland na Umoja wa Mataifa (UN).

RC ataka mikataba afua za lishe itekelezeke
Sababu madhara ya afya kwa Wanawake na Watoto zatajwa