Waziri Mkuu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imeamua kufufua mazao matano ambayo yanaingiza kwa wingi fedha za kigeni nchini.

Amesema kuwa Serikali imeamua kuboresha mazao ya tumbaku, chai, kahawa na pamba ili yaweze kuwanufaisha wananchi.

Ameyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi kwenye maeneo mbalimbali akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora.

Aidha, amesema kuanzia sasa serikali imepiga marufuku matumizi ya dola za Marekani kwenye ununuzi wa zao la tumbaku kwa sababu mazao mengine makuu hapa nchini yananunuliwa kwa fedha za Kitanzania.

“Ni kwa nini tumbaku inunuliwe kwa dola za Marekani ilhali mazao mengine yananunuliwa kwa fedha za Tanzania? Korosho, pamba, chai na kahawa, wakulima wetu kote huko wanalipwa kwa fedha za Tanzania, kwa nini tumbaku iwe tofauti?” alihoji  Majaliwa.

Hata hivyo, Majaliwa amewataka watendaji na watumishi wa Halmashauri na wilaya za mkoa wa Tabora wasimamie zao la tumbaku ili kuinua kilimo cha zao hilo na kuwanufaisha wakulima.

 

Prof. Mbarawa atoa mwezi mmoja kwa wafanyabiashara kulipa kodi
Mbowe: Kilimanjaro hatutegemei CCM kuleta maendeleo