Viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, likiwemo la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, kazi Duniani ILO na la kuhudumia watoto UNICEF, wametoa ujumbe wa pamoja kwa kunukuu msemo ya kwamba huwezi kufundisha leo kama ulivyofundisha jana ili kuandaa wanafunzi wa kesho.

Nukuu hiyo ya John Dewey, imetolewa na Viongozi hao ambao ni Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu ILO Gilbert F. Houngbo na Mkurugenzi Mtendaji UNICEF, Catherine Russell ambao wamesema wanatambua umuhimu wa marekebisho ya mfumo wa elimu ili uweze kumuandaa mtoto kukabiliana na mabadiliko ya Dunia.

Kupitia ujumbe wao wa pamoja wamesema, “Dunia imeazimia kurekebisha mfumo wa elimu na kushughulikia vikwazo vikuu vinavyozuia walimu kuwa viongozi wa marekebisho hayo na mustakabali wa elimu unatoa wito kwa mkataba mpya wa kijamii na elimu, ambamo kwao walimu ndio kitovu cha marekebisho na tasnia yao inayotathminiwa na kufikiriwa upya.

Aidha, Bila kazi ya walimu haiwezekani kutoa elimu jumuishi, yenye usawa na bora kwa kila mwanafunzi. Wao ni muhimu katika kujikwamua baada ya janga la Uviko-19 na kuandaa wanafunzi wa zama zijazo na kwamba bila ya kurekebisha mazingira ya kazi wanamofanyia walimu, ahadi ya elimu ya kukabili mabadiliko ya dunia itasalia kuwa ni ndoto isiyofikiwa.

Jaribio Kombora la Korea Kaskazini, Mataifa tumbo joto
Uchochezi: Wanahabari waachiliwa huru baada ya miaka minne kizuizini