Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu yenye Makao makuu yake Jijini Arusha, imeonyesha kuguswa na mabinti ambao ni waathirika wa mimba za utotoni, ndoa za utotoni na umasikini kwa kuitaka jamii kutowatenga badala yake iwasaidie kuzifikia ndoto zao

Rais wa Mahakama ya Afrika, Jaji Imani Aboud ameeleza hayo wakati mahakama hiyo ilipowatembelea Mabinti hao wanaolelewa katika Taasisi Ya Faraja ambayo huwapokea na mabinti hao na kuwarejesha shuleni Pamoja na kuwapa stadi za Maisha.

Jaji Imani Aboud amewataka Mabinti hao kutokukata tamaa, badala yake wajifunze kwa taliyopita na kusonga mbele huku akiiasa jamii kuwapa ushirikiano.

Rais wa Mahakama ya Afrika Jaji Imani Aboud

”Ni ukweli usiopingika kuwa wanawake ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi maana wasiposhirikiswa na kuwekewa mazingira wezeshi jamii yoyote ile haiwezi kuendelea kikamilifu” amesema Jaji Imani

”Hivyo basi ninawasihi kila mmoja wenu achochee mabadiliko kwa kutoa vipaumbele katika maswala yanayowahusu wanawake katika program za miradi mbalimbali na kuleta usawa wa kijinsia na kuharakisha maendeleo ya watu wote kwa ujumla” amesema Jaji Imani .

Hata hivyo Mahakama hiyo imetoa msaada wa Vifaa mbalimbali kwa mabinti hao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Faraja Estar Mushi amesema zaidi ya mabinti 500, waliopata mimba za utotoni na kushindwa kuendelea na masomo wamesaidiwa na taasisi hiyo

Serikali yasitisha vibali ukarabati Majengo chakavu
Dkt. Yonazi azungumza na Menejimenti ya Tume TACAIDS